05. Tofauti ya mtu mwenye azma na mvivu katika Ramadhaan

Swali 5: Watu wengi katika Ramadhaan hamu yao kubwa imekuwa ni kuleta chakula na kulala. Kwa watu hawa Ramadhaan imekuwa ni mwezi wa uvivu na kutokuwa na la kufanya. Ni kama ambavo baadhi yao wanakesha usiku wanacheza na wanalala mchana. Ni zipi nasaha zako?

Jibu: Naona kuwa kufanya hivi ni kupoteza wakati na pesa. Ikiwa watu hawana hamu nyingine isipokuwa kuleta makulati mbalimbali, kulala mchana, kukesha usiku juu ya mambo yasiyowanufaisha, hapana shaka kwamba mambo haya ni kupoteza fursa yenye thamani ambayo pengine isimrudilie tena mtu katika maisha yake.

Mtu mwenye azma ni yule ambaye anapita katika Ramadhaan kwa mujibu wa vile inavyotakikana katika kulala mwanzoni mwa usiku baada ya kuswali Tarawiyh na kuswali mwishoni mwa usiku ikimuwepesikia kufanya hivo. Kadhalika hafanyi israfu katika vyakula na vinywaji.

Aidha inatakikana kwa yule mwenye uwezo kupupia kuwafuturisha wafungaji ima misikitini au maeneo mengineyo. Kwa sababu ambaye anamfuturisha mfungaji anapata mfano wa ujira wake. Mtu akiwafuturisha ndugu zake wafungaji basi anapata mfano wa thawabu zao. Kwa hivyo yule ambaye Allaah amemtajirisha anatakiwa kuchuma fursa hii ili apate ujira mwingi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 13
  • Imechapishwa: 11/04/2021