05. Sura ya tatu: Njia za kuepuka kupinda kutoka katika ´Aqiydah sahihi

Njia za kuepuka upondokaji huu zimefupika katika yafuatayo:

1- Kurudi katika Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) na katika Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kupokea ´Aqiydah sahihi kutoka katika viwili hivyo kama ambavyo as-Salaf as-Swaalih walivyokuwa wakichota ´Aqiydah zao kutoka humo. Hautofaulu mwisho wa Ummah huu isipokuwa kwa kile kilichofanya wa mwanzo wao kufaulu. Sambamba na hilo watu wasome ´Aqiydah za mapote yaliyopinda, kujua shubuha zao kwa ajili ya kuziraddi na kuyatahadharisha. Kwa sababu yule asiyejua shari kuna khatari akatumbukia ndani yake.

2- Kutilia umuhimu wa kuisoma ´Aqiydah sahihi – ambayo ni ya as-Salaf as-Swaalih – katika hatua mbalimbali za masomo na kuipa silebasi ya kutosha ya mifumo na kutilia umuhimu wa hali ya juu katika mitihani ya mada hii.

3- Viwekwe vitabu vya Salafiyyah iliosafi na viwekwe mbali vitabu vya mapote potofu kama Suufiyyah, wazushi, Jahmiyyah, Mu´tazilah, Ashaa´irah, Maaturiydiyyah na wengineo. Isipokuwa kuvijua kwa lengo la kuraddi yale yaliyomo na kuvitahadharisha.

4- Walinganizi wenye kutengeneza kusimama kidete kwa ajili ya kuwahuishia watu ´Aqiydah ya Salaf na waraddi upotevu wa wale waliopinda kutokamana na hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 14-17
  • Imechapishwa: 22/01/2020