05. Sifa ya pili ya mwanamke ili aweze kuitengeneza jamii

Sifa ya pili: Ubainifu na ufaswaha.

Allaah amtunuku mwanamke kuweza kubainisha na ufaswaha kwa njia ya kwamba awe na ufaswaha wa ulimi na kauli ya kujieleza kwa njia ya kwamba aweze kuelezea yale yaliyomo kifuani mwake kwa njia ya ukweli. Afichukue ile maana iliyomo moyoni na ndani ya nafsi yake. Hiki ni kitu wanachoweza kuwa nacho wengi lakini hata hivyo wasiweze kukielezea. Pengine wakaweza kukielezea lakini hata hivyo ikawa kwa maelezo yasiyokuwa ya wazi na yenye kuathiri. Katika hali hiyo hakutofikiwa lengo liliyomo moyoni mwa yule mzugumzaji ambalo ni kuwarekebisha viumbe. Kujengea juu ya hili tunapenda kuuliza ni sababu gani zinazomfikisha mtu katika hili; kuweza kubainisha, ufaswaha na kuelezea yale yaliyomo ndani ya nafsi kwa ibara za kweli zenye kuweka wazi yale yaliyomo kifuani? Hilo litaweza kufikiwa pale ambapo mwanamke atakuwa na kitu kidogo katika elimu ya kiarabu; sarufi na balagha yake. Hapo atalazimika mwanamke kuyasoma hayo japo kidogo kwa njia ya kwamba aweze kuelezea yale yaliyomo nafsini mwake kwa maelezo sahihi kwa njia ya kwamba anaweza kufikia lile lengo kwenye mioyo ya wanawake anaowazungumzisha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017