Ndio maana nikasema tunatakiwa kutilia umuhimu kuutambua mfumo wa Salaf na kuusoma inapokuja katika ´Aqiydah, tabia na mambo ya kijamii. Inapokuja katika mambo yote. Salafiyyah ndio mfumo aliokuwemo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah wake katika al-Muhaajiruun na al-Answaar (Radhiya Allaahu ´anhum) na waliofuata uongofu wao mpaka Qiyaamah kisimame. Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakitoacha kipote katika Ummah wangu… “

Hawa ndo Salafiyyuun.

“… kuwa juu ya haki na wenye kushinda. Hawatowadhuru wale wenye kuwapinga na wenye kwenda kinyume nao mpaka ifike amri ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).”

Maneno yake (´alayhis-Swalaatu was-Salaam):

“Hawatowadhuru wale wenye kuwapinga na wenye kwenda kinyume nao… “

Inafahamisha kuwa kutakuwa wenye kwenda kinyume nao na wenye kuwapinga, lakini hata hivyo hawajali. Yeye anafuata njia ya kumfikisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) na wakati huo huo anastahamili yale yenye kumsibu. Luqmaan alimwambia mwanawe na huku akimpa mawaidha:

يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنكَرِ وَاصْبِرْ عَلَى مَا أَصَابَكَ إِنَّ ذَلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ وَلَا تُصَعِّرْ خَدَّكَ لِلنَّاسِ وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ مُخْتَالٍ فَخُورٍ وَاقْصِدْ فِي مَشْيِكَ وَاغْضُضْ مِن صَوْتِكَ إِنَّ أَنكَرَ الْأَصْوَاتِ لَصَوْتُ الْحَمِيرِ

“Ewe mwanangu! Simamisha swalah, na amrisha mema, na kataza maovu na subiri kwa yanayokupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. Wala usiwabeuwe watu, wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika Allaah Hampendi kila anayejivuna na kujifakhirisha. Na ushike mwendo wa katikati na teremsha sauti yako. Hakika katika sauti mbaya zote bila ya shaka iliyozidi ni sauti ya punda.” (31:17-19)

Huu ndio mfumo wa Salaf. Hizi ndizo alama na sifa zao. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَأَنَّ هَـذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Hii ndio Njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni na wala msifuate njia za vichochoro vitakufarikisheni na Njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kuwa na taqwa.” (06:153)

Maneno Yake (Ta´ala):

وَأَنَّ هَـذَا صِرَاطِي

“Hii ndio Njia Yangu… “

Ameinasibisha Kwake Mwenyewe. Unasibishaji wa kujitukuza Yeye na yule mwenye kuifuata:

وَأَنَّ هَـذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ

“Hii ndio Njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni na wala msifuate njia za vichochoro… ” (06:153)

Ni dalili ya kuonesha kuwa kuna njia za vichochoro. Hakuviwekea kikomo. Ni vichochoro vingi.

وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ

“… na wala msifuate njia za vichochoro… “

Huu ndio mfumo wa makundi yanayoenda kinyume na mfumo wa Salaf.

وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“… na wala msifuate njia za vichochoro vitakufarikisheni na Njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kuwa na taqwa.”

Ameanza (Subhaanah) kwa kusema:

فَاتَّبِعُوهُ

“… ifuateni… “

Halafu akasema:

ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kuwa na taqwa.”

Huenda kwa kufanya hivo mkamcha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), kuogopa upotevu, utata na kuogopa vizuizi vilivyoko katika kuifikia Njia hii. Ni dalili yenye kuonesha kuwa mtafikwa na mambo. Tazama namna Alivyoifanya Njia Yake kuwa moja na Akafanya njia za vichochoro kuwa vingi! Njia ya Allaah iliyonyooka ni moja peke yake na sio nyingi. Kuhusiana na vichochoro ni vingi havihesabiki. Kila mmoja amejichukulie njia na mfumo anaoufuata yeye na wafuasi zake. Kwa hivyo vichochoro ni vingi:

وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ

“… na wala msifuate njia za vichochoro… “

Aendapo mtafanya hivyo kutatokea nini?

فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

”… Vitakufarikisheni na Njia Yake.”

Vitakutoeni katika Njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Mtatumbukia katika upotofu na maangamivu. Hivyo hakuna uokovu, wema na mafanikio isipokuwa kwa kulazimiana na Njia iliyonyooka. Hiyo ndio Njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Kila yenye kwenda kinyume nayo ni njia ya shaytwaan. Katika kila njia hiyo kuna shaytwaan anayelingania watu kwazo kwayo. Tutahadhari na jambo hili. Tusidanganyike na na kubabaika na wingi wa wapinzani na utata. Usijali! Tufuate njia ya Allaah kwa ujuzi.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com