05. Salaf wote walikuwa wana imani moja

16- Muhammad bin Hamzah bin Abiys-Saqr ametukhabarisha: Abul-Hasan ´Aliy bin Ahmad bin Mansuur bin Qubays al-Ghassaaniy ametuhadithia: Baba yangu ametuhadithia: Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy amesema:

“Ahl-ul-Hadiyth wenye kushikamana na Qur-aan na Sunnah wanamtambua Mola wao (Tabaarak wa Ta´ala) kupitia sifa Zake zilizotajwa na Kitabu na Uteremsho Wake na kupitia wapokezi waadilifu na waaminifu kutokana na mapokezi yake Swahiyh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawaamini kuwa sifa Zake zinafanana na sifa za viumbe Wake. Hawazifanyii namna kama wafanyavyo Mushabbihah. Hawayapotoshi maneno kutoka mahala pake kama wafanyavyo Mu´tazilah na Jahmiyyah. Allaah amewakinga Ahl-us-Sunnah kutokamana upotoshaji na namna na akawatunuku uelewa na maarifa. Kwa njia hiyo wakawa wamehakikisha Tawhiyd na kumtakasia mapungufu na wakati huohuo wakaepuka ukanushaji na ufananishaji. Wanafuata maneno Yake (´Azza wa Jall):

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[1]

17- as-Swaabuuniy ametaja wale wanachuoni wanane na maimamu baada yao. Ametaja kwa majina idadi kubwa ya maimamu na akasema:

“Wote ni wenye kuafikiana. Hakuna baadhi waliowakhalifu wengine. Hakuthibiti kuwa kuna yeyote katika wao aliyepingana na tuloyasema.”[2]

[1] 42:11

[2] ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth (3).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ut-Ta’wiyl, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 01/05/2018