05. Ni lazima kwa mwanamke kwenda kuswali ´iyd

Huenda baadhi wakashangazwa na wanawake kutoka kwenda kuswali swalah ya ´Iyd uwanjani. Basi itambulike kuwa kitendo hichi ndio cha haki kisichokuwa na shaka yoyote ndani yake kutokana na Hadiyth nyingi zilizopokelewa juu ya jambo hili. Kwa sasa tutatosheka na kutaja Hadiyth ya Umm ´Atwiyyah iliyotangulia ambayo haionyeshi tu dalili kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah, bali ya kwamba ni wajibu. Kutokana na maamrisho yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na asli ya maamrisho yanaashiria uwajibu. Maoni hayo yanatiliwa nguvu na maneno ya Abu Bakr as-Swiddiyq ambaye amesema:

“Ni juu ya kila mwanamke mwenye shuka kutoka kwenda katika swalah za ´Iyd mbili.”[1]

Je, mtu ambaye anadai kuwanusuru makhaliyfah waongofu anasema hivi pia? Wakati wa mwanzo wao ameamrisha jambo hilo. Hatukuwadhania hivyo. Hivyo ima wathibitishe kuwa tumekosea, jambo ambalo tunalipendelea zaidi, vinginevyo itawabainikia watu kikweli kile wanachomaanisha pindi wanapodai eti wanawanusuru.

Kusema ya kwamba kitendo hicho ni wajibu, ni jambo lenye kusapotiwa na as-Swan´aaniy katika “Subul-us-Salaam”, ash-Shawkaaniy na Swiddiyq Hasan Khaan. Kadhalika ndio udhahiri wa maoni ya Ibn Hazm na ni kana kwamba Ibn Taymiyyah pia amemili kwayo katika “al-Ikhtiyaaraat” – na Allaah ndiye anajua zaidi.

[1] Ibn Abiy Shaybah katika “al-Muswannaf” (02/184). Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swalaat-ul-´Iydayn, uk. 12
  • Imechapishwa: 12/05/2020