05. Nguzo tano za Uislamu kwa watoto


Maana ya “Laa ilaaha illa Allaah” ni kwamba hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Na Ibraahiym alipomwambia baba yake na watu wake: “Hakika mimi najitenga mbali na yale mnayoyaabudu. Isipokuwa Yule Aliyeniumba, basi hakika Yeye Ataniongoa!” Na akalifanya neno [hili ni] lenye kubakia katika kizazi chake ili wapate kurejea.”[1]

Dalili ya kwamba ni wajibu kwa mtu kuswali na kutoa zakaah ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ

“Na hawakuamrishwa chochote kile isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye Dini kwa imani ilio safi, na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah. Na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara.”[2]

Kitu cha kwanza Allaah ameanza kusema katika Aayah hii ni kumuabudu Yeye peke yake na kujitenga mbali na shirki. Kitu kikubwa ambacho Allaah ameamrisha ni kumuabudu Yeye peke yake na kitu kiovu ambacho Allaah amekataza ni shirki. Allaah ameamrisha kusimamisha swalah na kutoa zakaah. Hicho ndio kitu kikubwa katika dini. Shari´ah nyenginezo zote ni zenye kuyafuata.

Dalili ya kwamba ni wajibu kwa mtu kufunga ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۚ فَمَن كَانَ مِنكُم مَّرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۚ وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ ۖ فَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ ۚ وَأَن تَصُومُوا خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ

“Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kufunga kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa. [Kufunga kwenyewe ni] siku za kuhesabika. Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini [akafunga baadhi ya siku], basi [akamilishe] idadi katika siku nyinginezo. Na ni juu ya wale wanaoiweza [kufunga] lakini kwa tabu watoe fidia; kulisha masikini. Na atakayejitolea kwa jema lolote lile basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu mkiwa mnajua! Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo. Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi mpya na afunge.”[3]

Dalili ya kwamba ni wajibu kwa mtu kuhiji ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا

“Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo.”[4]

[1] 43:26-28

[2] 98:05

[3] 02:183-185

[4] 03:97

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 2-7