05. Namna hii ndio tunaamini


Na sifa nyenginezo zote miongoni mwa khabari zisizokuwa wazi zilizosihi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Aayah za Qur-aan mfano wake tunatakiwa kukabiliana nazo kwa kuzikubali na wala hatuzirudishi nyuma wala kuzipindisha maana kama wanavofanya wale wanaokwenda kinyume, hatuzifananishi kama wanavofanya Mushabbihah na wala hatuzifasiri kwa lugha isiyokuwa ya kiarabu.

Hatuziashirii kwa mawazo ya moyo wala kwa mitikisiko ya viungo vya mwili. Bali tunatamka yale yaliyotamkwa na Allaah (´Azza wa Jall). Hatufasiri isipokuwa kile kilichofasiriwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na wale waliowafuata kwa wema na maimamu wa Salaf waliokuwa wakitambulika kwa dini na uaminifu. Tunaafikiana na kile walichoafikiana na tunanyamazia kile walichonyamazia.

Tunajisalimisha na khabari na Aayah kwa udhahiri wake zilivyoteremka na wala hatuonelei upindishaji maana wa Mu´tazilah, Ash´ariyyah, Jahmiyyah, Mulhidah, Mujassimah, Mushabbihah, Karraamiyyah na Mukayyifah.

Tunazikubali pasi na kuzipindisha maana na tunaziamini bila ya kuzifanyia mfano. Tunasema kuwa Aayah na khabari ni sahihi. Ni wajibu kuyaamini, kuonelea hivo ndio ´Aqiydah na kutafuta kuzipindisha maana ni Bid´ah na uzandiki.

Mwisho. Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhammad, kizazi chake, Maswahabah zake na wakeze.

  • Mhusika: Imaam Abul-Qaasim Sa´d bin ´Aliy bin Muhammad az-Zinjaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ajwibah fiy Usuul-id-Diyn, uk. 86-87
  • Imechapishwa: 15/06/2021