05. Mpangilio mzuri wa vitabu kwenye kabati kunaonyesha namna mwanafunzi anavyoijali elimu   

Adabu ya kwanza ni yeye apange vitabu vyake kwenye kabati ya vitabu. Mpangilio wa vitabu unaonyesha jinsi mwanafunzi anavyojali vitabu vyake. Vitabu vyake kuwa katika hali ya vurugu ni jambo lenye kuashiria mambo mawili:

1- Anatafiti na kusoma sana kwa kiasi kwamba vitabu vinatapakaa kila mahali. Ni sifa nzuri lakini hata hivyo anatakiwa baada ya hapo avipange.

2- Yeye mwenyewe asli yake ni mtu wa vurugu.

Haafidhw Ibn Hajar ametaja katika kitabu chake “Raf´-ul-Isr ´an Qudhwaati Misri” Qadhiy mmoja Misri aliyekuwa akikaa chumbani kwake hali ya kupanga vitabu vyake kwa mpangilio uliokuwa mzuri. Siku moja akajiwa na mwanafunzi na akamsifu namna alivyopanga vitabu vyake. Haafidhw Ibn Hajar akasema kuwa anaashiria kwamba kupanga vitabu ni jambo lenye kufahamisha kuwa havisomwi na mtu hastafidi navyo. Qaadhiy huyo akaelewa anachokusudia lakini akawa amenyamaza. Wakati mtu huyo huyo alipopata kazi kama mthibitishaji wa masuala ya ndoa Qaadhiy yule akaona namna alivyokosea katika suala la ndoa na akatumia fursa hiyo ya kumkemea kwa ukali mno kutokana na vile alivyomwambia. Kinacholengwa hapa ni kuwa anataka kusema mpangilio mzuri unaashiria kuwa vitabu havisomwi. Hili halina maana kuwa daima mambo yanakuwa hivyo. Pindi mwanafunzi anapotaka kutafiti jambo fulani anatoa vitabu kutoka pande mbali mbali na wakati anapomaliza anavirudisha mahali pake ili aweze kuvirejea kwa urahisi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Twaalib-ul-´Ilm wal-Kutub
  • Imechapishwa: 03/05/2020