05. Misingi ya sampuli za kuritadi


Kuritadi ni kurejea. Mwenye kuritadi ni yule anayerejea kutoka katika dini yake. Afanye hivo ima kwa maneno, kuamini, kitendo au kwa kuwa na mashaka. Hii ndio misingi ya aina za kuritadi. Kunatawanyika kutoka katika misingi hii sampuli nyingi katika vitenguzi vya Uislamu.

Kuna baadhi ya wajinga au wapuuzi wanapinga mtu kuzungumzia katika kubainisha sababu zinazopelekea katika kuritadi kutoka katika Uislamu na wanamsifu yule mwenye kufanya hivo kwamba ni “Takfiyriy” au wanafikia mpaka kutahadharisha naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 17-20
  • Imechapishwa: 03/05/2018