05. Mauaji na uporaji wa makundi yaliyojihami kwa silaha ni mfano wa ugaidi

4- Kwa hiyo yale matendo yanayofanywa na makundi yaliyojihami kwa silaha ambayo yanadai kuwa wako katika Jihaad na kwamba wanapambana ili kurudi katika Shari´ah ya Kiislamu ambapo wanawaua watu hawa, wanawapora wale, wanazitisha familia na jamii na kuyaharibu maduka na mashirika, viwanja vya ndege na masomo, ni mfano wa ugaidi wenye kutisha na uliofunikwa na matendo ya jinai yenye chuki, makubwa makali.

Licha ya hivyo watu hawa wanaojiita hivi na vile, wanadai kuwa wao ni wajuzi na wenye kutoa fatwa zinazoruhusu kuwaua watawala, pamoja vilevile na watu walionyamaza kimya juu ya madhambi ya watawala na hawawafanyii uasi, kutilia bidii kueneza Uislamu. Laiti wangelitumia juhudi zao kueneza ´Aqiydah ya Kiislamu, ´ibaadah, matendo, tabia, suluki na adabu kati ya watu kwa kiasi cha wanavyoweza. Wangelichukua mfumo wao kutoka katika Qur-aan tukufu na namna ya kuishi kwao kutoka katika Sunnah sahihi. Haya ndio walotakiwa kufanya kabla ya kuwatolea watu silaha zao, kuzitisha njia zao wanazopita na kutikisa usalama na utulivu wao. Matendo yao ni ukandamizaji, dhuluma na uadui, lakini wanasema kuwa wanafanya hivo kwa sababu ya kuwa na ghera juu ya Shari´ah ya Kiislamu na kwa ajili ya manufaa ya Ummah wa Kiislamu. Kwa njia hiyo wanaupaka rangi nyeusi Uislamu wa kweli. Wanafungua njia za matusi. Wanawafungulia njia maadui wa Uislamu na wa waislamu ulimwenguni kote. Wanasema kuwa Uislamu wetu mkuu ni mshenzi, ukandamizaji, upetukaji mipaka na ugaidi. Wanawahukumu waislamu wote hukumu moja na wanawaita kuwa ni magaidi na wapindukaji. Hawaheshimu haki yoyote ya uanaadamu. Yote haya yanatokamana na matokeo ya ulinganizi mbaya. Viumbe wanatakiwa kuitwa kwa njia sahihi na iliyowekwa katika Shari´ah inayoafikiana na mfumo wa wazi wa Mitume na Manabii.

Mimi nasema bila ya shaka ya kwamba watu hawa ni wapotevu katika kutangamana kwao na watu, pasi na kujali ngazi zao. Kwa ujumla hakuna yeyote aliyesalimika na shari zao. Hakuna hata mmoja aliyesalimika isipokuwa tu wale walioshikamana na taasisi za vikundivikundi na za kiharakati zinazobomoa na wala hazijengi, zinazoharibu sana na wala hazitengenezi.

Wanachuoni wengi wa Salafiyyah na waislamu wenye busara na wenye uoni wa mbali wamewaita na kuwatahadharisha kwa matendo yao mabaya wanayoyafanya kwa kutumia jina la Kiislamu la kulingania. Wanaua, wanapora na wanashambulia vilivyoharamishwa hata kama wenyewe kufanyiwa hivo watakuwa ni manaswara waliopewa amani. Wanawaghuri vijana wapumbavu ili waweze kuwachochea. Matokeo yake wanaingia ndani ya mashimo ya gereza bila ya kuhakikisha ulinganizi wa haki. Kwa kuwa walichofanya si cha sawa.

Pengine wakamtuhumu yule anayewatakia kheri na anayejua namna kunavyotakiwa kulinganiwa katika Uislamu ya kwamba anafanya kazi na serikali, mpakaji mafuta, mwoga, hajui mambo ya kisasa na anapuuzia dhiki zilizonazo Uislamu na waislamu. Watu kama hawa hawasikii. Hakufidishi kitu kuwanasihi. Wao ni kama yale maneno ya mshairi:

Ungelisikia lau ungelimwita aliye hai

lakini hana uhai yule unayemwita

Kile unachopuliza ndani yake ingelikuwa ni moto kingeliangaza

lakini kile unachopuliza ndani yake ni majivu

Msimamo wao kwa wale wanachuoni na wale wenye kuwatakia kheri na wenye hekima, wakweli na wenye ikhlaasw ni kama mshairi alivosema:

Msimamo wa mpumbavu kwa yule mwanachuoni

ni kama msimamo wa mwanachuoni kwa yule mpumbavu

Mmoja anajitenga mbali na yule mwengine

na huyu anajitenga mbali zaidi kuliko yule wa mwanzo

Naweza kusema ya kwamba lau kila mmoja angelilingania katika Uislamu kama walivyofanya Salaf ambao waliwafuata Manabii na Mitume, basi Allaah angewafanya watu wengi kuingia katika Uislamu kwa kutaka kwao wenyewe na kwa khiyari:

فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا

“Imani safi na ya asili ambayo Allaah amewaumbia kwayo viumbe.”[1]

Lakini watu hawa wamechagua njia nyingine mbali na ile iliyopitwa na wanachuoni wa Salaf na wafuasi wao. Hawakufikia kitu chochote katika yale wanayoyatilia bidii. Allaah peke yake ndiye anajua malengo na nia zao. Hali zao haziko mbali na yale maneno ya mshairi aliyesema:

Hivi kweli unatarajia kuokoka ilihali hukupita njia zake?

Boti halipiti nchikavu

[1] 30:30

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 12-14
  • Imechapishwa: 03/04/2017