05. Mapendekezo ya al-Awzaa´iy ni ngeni na dhaifu

Kuhusu al-Awzaa´iy kupendekeza kufanywa na mtu mmojammoja na Haafidhw Ibn Rajab kuchagua maoni haya ni maoni geni na dhaifu. Kwa sababu kila kitu ambacho hakikuthibiti kwa dalili za ki-Shari´ah ya kwamba kimewekwa katika Shari´áh basi haitofaa kwa muislamu kukizua ndani ya dini ya Allaah. Ni mamoja kimefanywa na mtu mmojammoja au kwa pamoja. Ni mamoja kimefanywa kisiri au kimetangazwa. Hilo ni kutokana na kuenea kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayefanya kitendo ambacho hamna ndani yake dini yetu atarudishiwa.”

Zipo Hadiyth nyenginezo zinazokemea na kutahadharisha Bid´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 26
  • Imechapishwa: 17/01/2022