05. Lulu kuhusu Abu ´Aliy an-Naysaabuuriy


5- Abu ´Aliy an-Naysaabuuriy (kfrk. 349) tabaka 11

adh-Dhahabiy ameandika wasifu wake katika “Tadhkirat-ul-Huffaadhw” na akasema:

“Imaam na Muhaddith wa Uislamu al-Husayn bin ´Aliy bin Yaziyd bin Daawuud an-Naysaabuuriy. Mmoja katika wakubwa wa Hadiyth.”

al-Haakim amesema:

“Alikuwa ni mtu wa kipekee inapokuja katika hifdhi, fahamu, uchaji, kudurusu na utunzi.”

Alizaliwa 277. Mara ya kwanza kusikia Hadiyth alikuwa na miaka mine. Kipindi alipokuwa mdogo alipokuwa akijishughulisha na uandishi. Pindi baadhi ya wanachuoni walipoona alivyo na akili wakamnasihi kutafuta elimu.”

Abu ´Abdir-Rahmaan as-Sulamiy amesema:

“Nilimuuliza ad-Daaraqutwniy kuhusu Abu ´Aliy an-Naysaabuuriy akasema: “Imaam mwenye kusafisha.”

Ibn Mandah amesema:

“Nilimsikia Abu ´Aliy an-Naysaabuuriy (na sijawahi kuona mtu mwenye hifdhi kama yake): “Hakuna kitabu chini ya mbingu kilicho sahihi zaidi kama “as-Swahiyh” ya Muslim.”

Abu Bakr al-Abhariy amesema:

“Nilimsikia Abu Bakr bin Daawuud akimuuliza Abu ´Aliy an-Naysaabuuriy: “Ibraahiym ni nani kutoka kwa Ibraahiym kutoka kwa Ibraahiym?” Akasema: “Ni Ibraahiym bin Twahmaan kutoka kwa Ibraahiym bin ´Aamir al-Bajaliy kutoka kwa Ibraahiym an-Nakha´iy.” Akasema: “Safi sana, Abu ´Aliy!”

al-Haakim amesema:

“Nilimsikia Abu ´Aliy an-Naysaabuuriy akisema: “Sijawahi kumuona mtu katika maswahibu zetu kama al-Ja´abiy. Hifdhi yake inanishangaza.” Nilisema hivo kumwambia Abu Bakr ambapo akasema: “Hivo ndivo anavosema Abu ´Aliy ilihali ukweli wa mambo yeye ndiye mwalimu wangu.”

al-Haakim amesema:

“Alifariki katika Jumaadaa al-Uulaa 349.”

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tadhkiyr-un-Naabihiyn, uk. 43-45
  • Imechapishwa: 11/06/2019