06. Kufaa kula na kulala msikitini kwa anayefanya I´tikaaf

Suala la nne: Yanayobatilisha I´tikaaf

1- I´tikaaf inabatilika kwa yafuatayo:

a) Kutoka msikitini pasi na haja kwa makusudi ijapo utakuwa mchache muda wa kutoka kwake. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:

“Alikuwa haingii nyumbani isipokuwa kutokana na haja akiwa mwenye kukaa I´tikaaf.”[1]

Isitoshe kutoka kunamkosesha mtu kukaa katika I´tikaaf yake, jambo ambalo ni nguzo ya I´tikaaf.

b) Jimaa. Ingawa itafanyika usiku au jimaa imetokea nje ya msikiti. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ

“Na wala msichanganyike nao hali ya kuwa nyinyi ni wenye kukaa I’tikaaf  misikitini.”[2]

Jengine lililo na hukumu moja kama hiyo ni kumwaga manii kwa matamanio mbali na kufanya jimaa. Kama mfano wa punyeto na limetokea kwa kufanya romantiki na mke pasipokuwa kwenye uke wake.

c) Kutokwa na akili. I´tikaaf inaharibika kwa wendawazimu na kulewa. Kwa sababu mwendawazimu na mlevi sio miongoni mwa watu ambao ´ibaadah inawalazimu.

d) Hedhi na damu ya uzazi. Kwa sababu haifai kwa mwenye hedhi na aliye na damu ya uzazi kukaa msikitini.

e) Kuritadi. Kwani jambo hilo linakinzana na ´ibaadah. Aidha amesema (Ta´ala):

لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ

“Ukifanya shirki bila shaka yataporomoka matendo yako.”[3]

[1] al-Bukhaariy (2029).

[2] 02:187

[3] 39:65

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 170
  • Imechapishwa: 06/05/2021