05. Kosa la tano katika ´Aqiydah: Kutundika na kuvaa hirizi

5- Kutundika hirizi katika mifupa, shell na vyenginevyo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yule mwenye kutundika hirizi basi Allaah asimtimizie mambo yake. Yule mwenye kutundika basi Allaah asimfanye kuwa na raha na utulivu. Mwenye kutundika hirizi amefanya shirki.”

”Hakika matabano, hirizi na at-Tiwalah ni shirki.”

Hadiyth hizi zimejumuisha hirizi. Ni mamoja ya Qur-aan au ya kitu kingine. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakubagua kitu. Jengine ni kwa sababu hirizi ya Qur-aan ni njia inayopelekea mtu kutundika kitu kingine. Hivyo ni lazima kukataza zote kwa ajili ya kuziba njia za shirki, kuhakikisha Tawhiyd na kuzitendea kazi Hadiyth. Isipokuwa tu matabano. Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amevua katika zile ambazo hazina shirki. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hakuna neno kwa matabano muda wa kuwa hakutokuwa shirki.”

Isitoshe (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwafanyia matabano baadhi ya Maswahabah zake. Kwa hiyo matabano hayana neno. Ni miongoni mwa sababu za Kishari´ah ikiwa ni kutoka katika Qur-aan tukufu, Sunnah iliyosihi au maneno ya wazi ambayo ndani yake hamna shirki wala matamshi maovu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Akhtwaau fiyl-´Aqiydah, uk. 4-5
  • Imechapishwa: 23/07/2020