1- Kula na kunywa. Hayo ni baada ya kuingia alfajiri ya pili. Yule mwenye kula au akanywa kwa kutaka kwake mwenyewe, hali ya kuwa anakumbuka kuwa amefunga, pasi na kutenzwa nguvu, basi swawm yake inaharibika. Juu yake kuna matishio makali. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi Kisha timizeni funga mpaka usiku.” (02:187)

Ni lazima kwake kuilipa siku hiyo. Vilevile ni lazima kwake kutubia tawbah ya kweli, ajutie na ajivue [asirudi tena].

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 12
  • Imechapishwa: 11/04/2019