1- Mfungaji anashukuru neema za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ikiwa ni pamoja vilevile na Qur-aan.

2- Mja ameamrishwa kufunga ili kuyaepuka madhambi. Anaipa nafsi yake mazoezi kumtii Mola Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) na kujiepusha na kumuasi (´Azza wa Jall).

3- Ikiwa una pupa na una kiu cha maasi matamanio yako yanadhoofika. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi kongamano la vijana! Yule katika nyinyi mwenye uwezo na aoe. Hakika hilo linasahilisha kushusha macho na kuhifadhi tupu. Kwa ambaye hawezi na afunge. Hakika hiyo ni ngao.”[1]

Mfungaji anakuwa kama ngao kwa sababu inamkinga na njia za matamanio zinazoweza kumfanya mja kumuasi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

4- Tumbo lisilokuwa na kitu linazifanya njia za damu za shaytwaan kuwa finyu ambazo anapitiaeko.

5- Imepokelewa kuwa swawm ni afya njema kwa idhini ya Allaah (Ta´ala). Hivyo mtu akijizoeza na kufunga sana basi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anampa kitu kingine kwa njia ya kwamba mafuta na uchafu mwilini unaondoka. Kula na kunywa sana kunasababisha tumbo kuumwa na maradhi. Kwa ajili hiyo swawm ni nzuri kwa ajili ya afya njema.

6- Utawafikiria pia ndugu zako wahitaji na masikini walio na njaa na kusibiwa na matatizo mengine. Hivyo utaanza kuwaonea huruma.

Zote hizi ni hekima. Ilio muhimu zaidi ni kuifunganisha nafsi na kuipa mazoezi ili iweze kumtii Mola (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] al-Bukhaariy (1905) na Muslim (1400).

 

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Istiqbaal Shahri Ramadhwaan, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 09/06/2017