Kunaweza kuwepo baki ya matamanio mwanzoni mwa ujana. Mzee atalipwa kwa kiasi cha subira yake. Kila ambavyo mtu anazidi kuzeeka ndivyo matamanio yake yanavyozidi kudhoofika na hapo shauku ya madhambi inasita.

Mzee akikusudia dhambi basi ni muasi. Kwa sababu yale matamanio ya kuvutia yamekwisha. Kwa ajili hiyo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kiumbe anayechukiwa zaidi na Allaah ni mzee mzinifu.”

Kuna wale wanaokusudia kuasi ili waweze kuvaa pete za dhahabu. Maangamivu kwa yule asiyezuiwa na mvi zake kutokamana na aibu zake! Hilo si kwa jengine isipokuwa tu amefanya hivo kwa sababu ya imani pungufu. Huenda mzee na mwanachuoni akasema kuwa elimu yake itamlinda. Anasahau kuwa elimu yake ni hoja dhidi yake. Kuliotwa kuhusu baadhi ya wazee wetu usingizini na namna walivyoambiwa:

“Allaah alikufanya nini?”

Ndipo wakasema:

“Amenisamehe na kunipa mgongo.”

Walipoulizwa juu ya hilo wakasema:

“Ndio, na vivyo hivyo inawahusu kundi la wanachuoni wasioitendea kazi elimu yao.”

Niliota kuhusu baadhi ya wazee wetu waliokuwa wazembeaji. Katika ndoto mtu huyo alikuwa uchi na mbwa watatu wadogo wamening´inia kifuani mwake ambapo mtoto wa mbwa ananyonya maziwa yao.

Aliotwa Yahyaa bin Aktham na namna alivyoulizwa ni kipi Allaah alichomfanya. Akasema:

“Alinambia: “Ee mzee muovu!”

Kadhalika Mansuur bin ´Ammaar.

al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mjinga anapata kusamehewa madhambi sabini kabla ya msomi kupata kusamehewa dhambi moja. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ

“Je, wanalingana sawa wale wanaojua na wale wasiojua?”[1]

Abud-Dardaa´ amesema:

“Maangamivu kwa yule anayetenda pasi na kujua mara moja! Maangamivu kwa yule anayejua na asitende mara saba!”[2]

Amesema vilevile:

“Kikubwa ninachokhofia ni pale nitakapoulizwa: “Ulitenda?” Nikisema: “Hapana”, basi nilitambua, na nikisema “Ndio”, basi hakuna Aayah yoyote inayoamrisha au kukataza isipokuwa ilitumiwa vibaya.”[3]

[1] 39:09

[2] az-Zuhd, uk. 176, ya Ahmad bin Hanbal.

[3] az-Zuhd, uk. 170, ya Ahmad bin Hanbal.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin al-Jawziy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyh-un-Naa’im al-Ghamr ´alaa Mawswim-il-´Umr, uk. 70-76
  • Imechapishwa: 15/02/2017