05. Hadiyth “Yule ambaye miguu yake itaingiwa na vumbi katika njia ya Allaah… “

687- Yaziyd bin Abiy Maryam amesema:

“Nilipokuwa natembea kuelekea swalah ya ijumaa nilimuwahi ´Abaayah bin Rifaay´ na nikasema: “Pata bishara njema! Hakika hatua zako hizi ni katika njia ya Allaah. Nimemsikia Abu ´Abs akielezea kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Yule ambaye miguu yake itaingiwa na vumbi katika njia ya Allaah imeharamishiwa Moto.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

al-Bukhaariy ameipokea kwa tamko:

“´Abaayah amesema: “Nilipokuwa natembea kuelekea swalah ya ijumaa Abu ´Abas aliniwahi na kusema: “Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Yule ambaye miguu yake itaingiwa na vumbi katika njia ya Allaah imeharamishiwa Moto.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Hakuna miguu ya mja inayoingiwa na vumbi katika njia ya Allaah halafu iguswe na Moto.”

Hapa hakuna maneno ya ´Abaayah kwa Yaziyd.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/431)
  • Imechapishwa: 02/02/2017