116- Abu Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Bwana mmoja alimjia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akimuomba ambapo akajibu: “Sina mimi cha kukupa. Lakini mwendee fulani.” Bwana yule akamwendea na akapewa. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Yeyote atakayeelekeza kheri basi ana mfano wa ujira wa yule mwenye kuifanya au mwenye kuitenda.”[1]

Ameipokea Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake. al-Bazzaar ameipokea kwa mukhtasari:

“Yeyote atakayeelekeza kheri basi ni kama mwenye kuitenda.”

117- Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr” na “al-Awsatw” kupitia kwa Sahl bin Sa´d[2].

[1] Swahiyh.

[2] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/158)
  • Imechapishwa: 03/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy