149- Jaabir bin ´Abdillaah ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tahadharini kupiga kambi katika njia… [1], kwa sababu huko ndio kimbilio la majoka na wanyama wakali, na kukidhi haja juu yake, kwa sababu kunasababaisha kulaaniwa.”[2]

Ameipokea Ibn Maajah na wapokezi wake ni waaminifu.

[1] Katika ile ya asili imekuja: ”… na kuswali juu yake… ”Nimeifuta kwa sababu sentesi hiyo amepwekeka nayo mpokezi ambaye ni dhaifu. Tazam “as-Swahiyhah” (2433).

[2] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/172)
  • Imechapishwa: 10/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy