05. Hadiyth “Swawm ni ngao dhidi ya Moto… “

982- ´Uthmaan bin Abiyl-´Aaswiy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Swawm ni ngao dhidi ya Moto, kama ngao zenu dhidi ya vita. Swawm nzuri ni kufunga siku tatu kila mwezi.”[1]

Ameipokea Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake[2].

[1] Swahiyh.

[2] Ameipokea vilevile Ahmad (4/22) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh pamoja vilevile na an-Nasaa´iy (1/311)  na (1/328) sehemu mbili tofauti. Ibn Maajah ameipokea bila ya ” Swawm nzuri ni… “.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (01/578)
  • Imechapishwa: 28/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy