05. Hadiyth “Huenda mfungaji hana kwa swawm yake zaidi ya kushinda njaa… “

1083- Vilevile amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Huenda mfungaji hana kwa swawm yake zaidi ya kushinda njaa. Huenda mwenye kusimama kuswali hana kwa kusimama kwake kuswali zaidi ya kukesha.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah na tamko ni lake, an-Nasaa’iy, Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” na al-Haakim ambaye amesema:

“Ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy.”

Matamshi yake ni:

“Huenda mfungaji fungu la swawm yake ni kushinda njaa na kiu. Huenda mwenye kusimama kuswali funga la swawm yake ni kukesha tu.”[2]

al-Bayhaqiy ameipokea kwa tamko lisemalo:

“Huenda mwenye kusimama kuswali funga la swawm yake ni kukesha tu. Huenda mfungaji fungu la swawm yake ni kushinda njaa na kiu.”[3]

[1] Nzuri kupitia zengine.

[2] Nzuri kupitia zengine.

[3] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/625-626)
  • Imechapishwa: 24/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy