Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

680- Salmaan bin ´Aamir adh-Dhabbiy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atapofuturu mmoja wenu basi afuturu kwa tende. Asipopata, basi afuturu kwa maji, kwani hakika hayo ni yenye kutwahirisha.”[1]

Wameipokea watano. Ameisahihisha Ibn Khuzaymah, Ibn Hibbaan na al-Haakim.

MAELEZO

Mfungaji anatakiwa kukata swawm kwa tende. Asipopata basi afuturu kwa maji. Hata hivyo tende tosa ni bora kuliko tende za kawaida. Mtu kwanza akate swawm kwa tende tosa, asipopata tende basi tende za kawaida, asipopata basi kwa maji. Asifuturu kwa mkate na mfano wake. Kitu cha kwanza kuingia tumboni mwake baada ya kufunga inatakiwa iwe tende tosa, tende za kawaida kisha maji. Hata kama atakuwa na vitu tamtam asivitangulize mbele ya maji, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyajaalia maji katika ngazi ya tatu. Asipopata vitu hivi vitatu au kinywaji chengine chochote, basi akate swawm kwa chochote anachotaka muda wa kuwa ni katika vile vilivyohalalishwa na Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Ahmad (4/16), Abu Daawuud (2355), an-Nasaa’iy katika “as-Sunan al-Kubraa” (3302), at-Tirmidhiy (657), Ibn Maajah (1699), Ibn Khuzaymah (2067), Ibn Hibbaan (3514) na al-Haakim (1/431).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mukhtaswar ´alaa Buluugh-il-Maraam (2/410-413)
  • Imechapishwa: 24/04/2020