05. Hadiyth ”Allaah amweke mbali yule ambaye atakutana na Ramadhaan… ”


996- Maalik bin al-Hasan bin Maalik bin al-Huwayrith amesimulia kutoka kwa baba yake ambaye na yeye amesimulia kutoka kwa baba yake akisema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipanda juu ya mimbari na akasema katika daraja ya kwanza: ”Aamiyn.” Halafu akasema katika daraja ya pili: ”Aamiyn.” Halafu akasema katika daraja ya tatu: ”Aamiyn.” Kisha akema: ”Jibriyl amenijia na akasema: ”Ee Muhammad! Allaah amweke mbali yule ambaye atakutana na Ramadhaan na asisamehewe!” Nikasema: ”Aamiyn.” Akasema: ”Allaah amweke mbali yule ambaye atawadiriki wazazi wake wawili, au mmoja katika wao, halafu akaingia Motoni!” Nikasema: ”Aamiyn.” Akasema: ”Allaah amweke mbali yule ambaye jina lako litatajwa mbele yake na asikuswalie.” Nikasema: ”Aamiyn.”[1]

Ameipokea Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh”.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/584)
  • Imechapishwa: 13/05/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy