05. Dalili ya tatu kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


3- ´Abdullaah bin Muhammad ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy bin Zakariyyaa at-Twuraythiythiy: Abul-Qaasim Hibatullaah bin al-Hasan at-Twabariy (yaani. al-Laalakaa’iy) ametuhadithia: Ahmad bin ´Ubayd ametuhadithia: ´Aliy bin ´Abdillaah bin Mubashshir ametuhadithia: Ahmad bin Sinaan ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: al-Mas´uudiy ametuhadithia, kutoka kwa ´Awn bin ´Abdillaah, kutoka kwa nduguye ´Ubaydullaah bin ´Abdillaah bin ´Utbah, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesema:

“Kuna mwanaume alimjia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mjakazi mweusi ambaye hakuwa mwarabu na akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ninalazimika kuacha mtumwa huru muumini.”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Allaah yuko wapi?”Akaashiria kwa kidole chake mbinguni. Kisha akamwambia: “Mimi ni nani?”Akaashiria kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha mbinguni. Kwa msemo mwingine wewe ni Mtume wa Allaah. Ndipo akasema: “Mwache huru.”[1]

Ameipokea Ahmad na al-Qaadhwiy al-Barqiy katika “al-Musnad” zake.

[1] Ahmad (3/450), Maalik (2/777) na Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhyd”, uk. 123. adh-Dhahabiy amesema:

”Hadiyth ni nzuri.” (al-´Uluww, uk. 17)

al-Albaaniy amesema:

”Katika mlolongo wa wapokezi kuna al-Mas´uudiy ambaye anaitwa ´Abdur-Rahmaan bin ´Abdillaah bin ´Utbah bin Mas´uud al-Kuufiy. Kumbukumbu yake ilichanganyikana. Hadiyth hii aliipokea baada ya kuwa kumbukumbu yake imeshachanganyikana. Yaziyd bin Haaruun ameipokea kutoka kwake. Ibn Numayr amesema: ”Alikuwa mwaminifu na mwishoni mwa uhai wake kumbukumbu yake ilichanganyikana. Ibn Mahdiy na Yaziyd bin Haaruun walisikia kutoka kwake Hadiyth zilizochanganyikana. Kwa ajili hiyo adh-Dhahabiy kusema ”Hadiyth ni nzuri” sio maneno mazuri.” (Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 81)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 69
  • Imechapishwa: 26/02/2018