Unadai:

“Hivyo nikaanza kulinganisha kati ya kichwa cha khabari na mada na kuona kuwa haviendani. Kwa ujumla inahusiana na vichwa vya khabari vya kushtua ambavyo vinamfanya msomaji kumtukana Sayyid Qutwub (Rahimahu Allaah). Kuhusiana na msomaji aliye angalau na uelewa mdogo, atakuta athari ya kinyume pindi ataposoma maudhui ndani ya kitabu na kwa ajili hiyo anarudi kuwa na mapenzi kwa vitabu vya Sayyid Qutwub (Rahimahu Allaah).”

Mosi: Hebu tulia, muheshimiwa Shaykh! Uhalisia wa mambo unatupilia mbali hukumu zako zinazopinda kutoka katika haki na zimeegemea katika batili na watu wake na zinavunjavunja mitazamo yako hii.

Watu ambao ni wajuzi zaidi yako na wenye uelewa mpana na walio na ufahamu wa kina kuliko wewe, hawakukutana na athari hii ya kinyume na himdi zote anastahiki Allaah. Wanachuoni hawa vigogo wamesoma kitabu na kuona kuwa mambo yanaendana. Hilo linatiliwa nguvu na fikira na I´tiqaad nyingi za Sayyid Qutwub ambazo ni upotevu juu ya upotevu na batili juu ya batili. Maandiko yake kwenye kitabu yanaonyesha batili ya wazi kabisa ambayo haiwezi kuonekana tu na ambaye ni mkaidi.

Baadhi ya wanachuoni vigogo hao, waliyoko ndani ya nchi na nje ya nchi, wameyasema hayo mdomo kwa mdomo wakati wa kukutana na kwenye mazungumzo ya simu. Wao – Allaah akitaka – ni katika mashahidi bora wa Allaah juu ya ardhi na ni katika wabora wa kundi lililookoka na kunusuriwa ambao hawadhuriki na wale wenye kuwakosesha nusura na wale wenye kwenda kinyume nao mpaka ifike ahadi ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).

Pili: Inaonekana kana kwamba unafurahishwa na watu kuwa na mapenzi juu ya vitabu vya Sayyid na wakati huo huo unashtushwa na mashambulizi ya Sayyid kwake mwenyewe, Uislamu na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Hivi kweli unafurahishwa na “al-´Adaalah al-Ijtimaa´iyyah” na yale mabalaa yanayopatikana ndani yake? Unafurahishwa na mapenzi ya watu, pasi na kujali kiwango cha uelewa walichonacho, juu ya “al-´Adaalah al-Ijtimaa´iyyah” ambacho kimejengwa juu ya midahalo mitatu yenye kuangamiza:

1- Ujamaa. Sayyid anapotosha maandiko ya Qur-aan na Sunnah na kanuni za Kishari´ah ili auhakikishe na kuulazimisha Ummah kwao.

2- Matusi ya khaliyfah mwongofu ´Uthmaan na wale Maswahabah na Taabi´uun bora kabisa waliokuwa wakieshi zama zake. Vilevile anaitukana dola ya Umayyah na kuitoa nchi hiyo na dola ya ´Abbaasiyyah kutoka katika mipaka ya Uislamu inapokuja katika hukumu na uchumi. Aidha anawasifia wale waliomfanyia uasi ´Uthmaan na kuonelea kuwa wao ni bora kuliko yeye na mambo mengine mengi.

3- Kuukufurisha Ummah wa Kiislamu.

Unafurahishwa na watu kuwa na mapenzi juu ya “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” ambayo imejaa I´tiqaad na fikira nyingi za kipotevu?

Unafurahishwa na watu kuwa na mapenzi juu ya “at-Taswiyr al-Fanniy” ambapo ndani yake amemshambulia Nabii mkubwa, kukanushwa kwa sifa za Allaah na kujiweka huru kutokamana na utakasifu wa Qur-aan? Soma anavyosema:

“Tunaweza kuweka kando utakasifu wa Qur-aan wa kidini kwa muda na vivyo hivyo malengo ya Da´wah ya Kiislamu.”[1]

Ni kutokea hapa na kujiweka huru kabisa kutokamana na utakasifu wa Qur-aan ambapo Sayyid Qutwub amemtukana Mtume wa Allaah Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kujifanya ni mjinga juu ya unabii wake na nafasi yake mbele ya Allaah na mbele ya waumini. Ameifanyia Qur-aan vibaya sana. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakuiteremsha Qur-aan isipokuwa ni ili imwongoze mwanaadamu katika uongofu wa kidini na wa Kiislamu na tabia na sio kwa ajili ya sanaa. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hayuko radhi na yeyote mwenye kuzungumzia uelewa, lugha ya Qur-aan au elimu nyingine yoyote baada ya kujiweka huru kutokamana na dini na utakasifu wa Qur-aan.

[1] at-Taswiyr al-Fanniy, uk. 24