05. Allaah ana khiyari nini atawafanya watenda madhambi

Kinacholengwa ni kwamba imani inashuka, inashuka na inashuka. Watu hawa wana imani dhaifu. Mtu asiyeswali ataadhibiwa vibaya sana. Wanachuoni wengi wamefikia mpaka kumkufurisha. Mmiliki wa ngamia ambaye hatoi zakaah atawekwa mahali pa mkusanyiko siku ya Qiyaamah ili ngamia zimkanyage na kumuuma. Mmiliki wa ng´ombe asiyetoa zakaah atakanyagwa na kupigwa mapembe na ng´ombe. Mmiliki wa kondoo asiyetoa zakaah atakanyagwa na kupigwa mapembe. Haya yatakuwa siku ambayo ni sawa na miaka 50.000[1].

Ahl-us-Sunnah wa kati na kati wanaieleza Qur-aan na kuiamini kama inavyotakikana na wanaiamini Sunnah na kuifuata, wanaonelea kuwa Allaah ana khiyari cha kuwafanya watenda madhambi. Akitaka kuwaadhibu, atawaadhibu, na akitaka kuwasamehe, atawasamehe. Atayeadhibiwa ataingia Motoni na ataadhibiwa vilevile mahali pa mkusanyiko siku ya Qiyaamah, kama ilivyo hali ya yule ambaye hatoi zakaah. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu mla ribaa:

الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ

“Wale wanaokula ribaa hawatosimama isipokuwa kama anavyosimama yule aliyezugwa na shaytwaan kwa kuguswa.” 02:275

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anamlaani mwenye kula ribaa, mwenye kuiandika na mashahidi wake wawili.” Muslim (1598).

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ

“Msipofanya hivo, basi tangazeni vita kutoka kwa Allaah na Mtume Wake.” 02:279

Amewahukumu kufuru pale aliposema:

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

“Atakayemuua muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Moto ni mwenye kudumu humo na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamwandalia adhabu kuu.” 04:93

Lakini ukafiri huu unawahusu wale wenye kuhalalisha.

Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah juu ya imani.

[1] al-Bukhaariy (1402) na Muslim (987).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 14-16
  • Imechapishwa: 09/10/2016