05. Adabu ya tano: Kula, kulala na kuzungumza kidogo iwezekanavyo


Kumetangulia maneno juu ya kwamba mwanafunzi inatakiwa chakula chake kinatakiwa kiwe cha halali na kidogo…

Kitendo cha chakula kuwa cha halali ni jambo linalotakikana kwa waislamu wote. Inapokuja kwa haki ya muislamu ni jambo limekokotezwa zaidi. Kwa kuwa mwanafunzi ni mtambuzi zaidi kwa kile ambacho ni halali na haramu. Kumetangulia maneno juu ya kuwa na unyenyekevu katika vyakula na vinjwaji na namna alivyoacha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tende aliokutana nayo juu ya kitanda chakula kwa kuchelea isije kuwa ya swadaqah, kwani swadaqah haijuzu kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mwanafunzi ni mwenye kushughhulishwa na yale aliyomo ya kujifunza kutokamana na kufikiria vyakula na vinywaji. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah haikusikika hata siku moja akiomba chakula, si chakula cha mchana wala cha jioni – pasi na kujali kubaki vitavyobaki – hilo ni kutokana na namna alivyokuwa ni mwenye kushughulishwa kwa hali ya juu ya na elimu na matendo. Bali wakati mwingine alikuwa akiletewa chakula na huenda akakiacha kikabaki kwa muda fulani mpaka akakigeukia. Na pale anapokula basi anakula kidogo tu. Hakuwa na tamaa na dunia. Hakuwa ni mwenye kuzungumzia mambo ya kidunia na kuuliza kitu juu ya maisha yake. Hamu yake kubwa ilikuwa ni Aakhirah na yenye kumkurubisha kwa Allaah (Ta´ala)…

Kuhusu kulala ni juu ya mwanafunzi kulala kidogo kiasi cha kwamba hatojisababishia madhara katika mwili na akili yake. Ndani ya masaa ishirini na nne asizidishe katika kulala kwake masaa manane. Ni theluthi ya zama. Hali yake ikimruhusu kulala chini ya hapo afanye hivo.

Kuhusu kuzungumza maneno madogo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye anamuamini Allaah na siku ya Mwisho, basi azungumze yaliyo mazuri au anyamaze.”[1]

Ibn ´Abdil-Barr (Rahimahu Allaah) amesema:

“Katika fitina za mwanachuoni ni maneno yawe yanapendeza kwake zaidi kuliko kusikiliza.” Maoni haya yamepokelewa kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb na amesema: “Katika kusikiliza kuna usalama na elimu zaidi. Msikilizani anashirikiana na mzungumzaji.” Amesema tena: “Katika maneno kuna ufikiriaji, upambaji, nyongeza na upunguzaji.” Amesema vilevile: “Hakika mzungumzaji kunasubiriwa kwake fitina na msikilizaji kunasubiriwa kwake rahmah.”

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Sa´iyd Raslaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadab Twaalib-ul-´Ilm, uk. 83-93
  • Imechapishwa: 23/04/2017