Unadai:

“Nasikitika kuona wanachuoni wa waislamu wa ulimwengu hawakuona makosa haya yenye kuangamiza. Ni vipi mtu anaweza kuoanisha hili na vitabu vya Sayyid Qutwub kuenea ulimwengu mzima?”

Wanachuoni wamegawanyika sehemu mbili; Ahl-us-Sunnah na Ahl-ul-Bid´ah.

Kuhusu Ahl-us-Sunnah – na wao ndio wanaozingatiwa – inaonekana kuwa hawakuvisoma na wala hawakufaidika navyo.

Wewe mwenyewe ulinambia kuwa ulisoma kitabu cha “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” pindi ulipokuwa sekondari na kwamba hukuweza kukisoma. Kwa hiyo ukakiweka kwenye kabati ya vitabu. Huko ndiko ulikiweka mpaka uliponieleza maneno haya. Kwenye makaratasi haya unasema:

“Naomba udhuru kwa jibu langu lenye kuchelewa. Hata kama vitabu vya mtu huyu vimeenea kati ya watu, hapo kabla sikutilia umuhimu wa kuvisoma.”[1]

Ni kwa nini hukutilia umuhimu wowote juu ya vitabu vya Sayyid Qutwub ilihali wewe ni mtu kabambe? Ni kwa nini “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” kibaki ndani ya kabati? Ni kwa nini hukukitilia umuhimu hata mdogo? Ni lazima kuwepo sababu na vikwazo vya ki-I´tiqaad na vya kimfumo juu hilo na vilevile njia za maajabu zinazotikisa ubongo wa msomaji. Ndio maana ulitakiwa kuwalinganisha wanachuoni wa Ahl-us-Sunnah na wewe mwenyewe na kujiweka ya kwamba hawajakisoma kama ambavyo wewe mwenyewe hujakisoma kutokana na sababu hizo hizo. Huenda vilevile wakawa na sababu zingine kama vile ujinga na upotevu wake. Kwa ajili hiyo wakawa wamevipuuza vitabu vyake. Lau wangevisoma, basi wangeona makosa yavyo ya kuangamiza na wangewatahadharisha watu navyo.

[1] Uk. 04