4- Mara nyingi huapa kwa jina la Allaah kwa uongo na ulaghai. Wanaona kwamba mwenendo huo unanufaisha Da´wah yao wanayolingania kwayo. Wanachomaanisha ni kwamba Da´wah zote ni zenye kuihitajia na yenyewe haihitajii kitu. Kwa sababu Da´wah yao imeasisiwa na Hasan al-Bannaa. Mmoja katika washairi wao amesema:

al-Ikhwaan wana mnara

Kila kilichomo humo ni kizuri

Usiulze ni nani aliyeujenga

Aliyeujenga ni Hasan[1][2]

[1] Huku ni kuwa na msimamo wa kuvuka mipaka kwa Hasan al-Bannaa, mfumo wake na mifumo ya wafuasi wake. Kitu kilicho kizuri kwa ukamilifu ni kile tu kilichomo katika Kitabu kitukufu cha Allaah na Sunnah Swahiyh kutoka kwa mkarimu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[2] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 25/03/2017