04. Vipange vitabu vyako kwenye kabati ya vitabu

Kabla ya kuingia katika adabu za jumla tunasema kuwa kule mwanafunzi kutilia umuhimu mkubwa juu ya vitabu vyake kunaonyesha anavyoitilia umuhimu elimu.

Moja katika adabu ambazo mwanafunzi anatakiwa kuzijali ni kwamba anatakiwa kupanga vitabu vyake ili imuwie rahisi kuvirejea. Ikiwa anataka angalia jambo fulani katika vitabu basi ni lazima avipange. Kupanga vitabu inatakiwa iwe kutokana na hali ya mwanafunzi huyu. Ikiwa anahitajia kupanga vitabu vya Tafsiyr ya Qur-aan vyote kivyake, vitabu vya Hadiyth vyote kivyake, vitabu vya Fiqh vyote kivyake kutokamana na madhehebu na kadhalika, ni sawa. Ikiwa anaonelea kuwa ananufaika zaidi na mpangilio mwingine, ni sawa pia. Yote hayo yanahusiana na yeye aweze kupata kitabu pale anapokihitajia.

Kuna aina mbili ya vitabu:

1- Vitabu vikubwa.

2- Vijitabu vidogo.

Vile vitabu vikubwa ataviona kwenye kabati ya vitabu kwa sababu ni vikubwa na vina mijaladi mikubwa, mijaladi kumi, mijaladi kumi na tano, mijaladi mitatu, mijaladi mine na kadhalika. Vi vyenye kuonekana.

Vitabu vidogo ndivyo vinavyohitajia kutiliwa umuhimu. Ndivyo vitabu muhimu na pengine vikawa na elimu isiyopatikana kwenye vile vikubwa. Endapo atataka kuangalia jambo fulani kwenye kitabu asilipate. Kwa nini asilipate? Kwa sababu amekiweka pahali pasipostahiki. Vijitabu hivi vidogo vinatakiwa kuwa sehemu tofauti. Havitakiwa kuwa kati ya vtabu vikubwa. Asiweki kijitabu kilicho na baadhi ya kurasa, kurasa arubaini au khamsini karibu na kitabu kikubwa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Twaalib-ul-´Ilm wal-Kutub
  • Imechapishwa: 03/05/2020