فإذا قيل لك: ما دينك؟

Swali 5: Ni ipi dini yako?

فقل : ديني الإسلام

Jibu: Dini yangu ni Uislamu.

ومعنى الإسلام: الاستسلام لله بالتوحيد والانقياد له بالطاعة وموالاة المسلمين ، ومعاداة المشركين
قال تعالى

Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah kwa kumpwekesha, kunyenyekea Kwake kwa kumtii, kuwapenda waislamu na kuwachukia washirikina. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

“Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu.”[1]

وقال

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake, naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[2]

وصح عن النبي إنه قال

Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

أنْ تَشْهَدَ أن لا إله إلا اللهُ وأنَّ محمداً رسولُ اللهِ ، وتُقيِمَ الصَّلاَةَ، وتُؤْتِيَ الزكاةَ، وتصومَ رمضان، وتحُجَّ البيتَ إن اسْتطعْتَ إليه سَبِلاً

“Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga ramadhaan na kuhiji ikiwa mtu ana uwezo wa kufanya hivo.”[3]

[1] 03:19

[2] 03:85

[3] al-Bukhaariy (4777) na Muslim (102).

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 16-18
  • Imechapishwa: 25/03/2017