04. Uislamu kwa watoto


Swali 5: Ni ipi dini yako?

Jibu: Dini yangu ni Uislamu. Uislamu maana yake ni kujisalimisha kwa Allaah kwa kumpwekesha, kunyenyekea Kwake kwa kumtii, kuwapenda waislamu na kuwachukia washirikina. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

“Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu.”[1]

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake, naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[2]

Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga ramadhaan na kuhiji ikiwa mtu ana uwezo wa kufanya hivo.”[3]

[1] 03:19

[2] 03:85

[3] al-Bukhaariy (4777) na Muslim (102).

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 16-18
  • Imechapishwa: 25/03/2017