04. Sifa ya kwanza ya mwanamke ili aweze kuitengeneza jamii

Ni lazima kwa mwanamke ajipambe kwa sifa maalum na atekeleze lile jukumu lake ili aweze kuhakikisha ule umuhimu wake wa kuitengeneza jamii. Zifuatazo ni baadhi ya hizo sifa:

Sifa ya kwanza: Wema wa mwanamke.

Mwanamke yeye mwenyewe anatakiwa kuwa mwema. Mwanamke anatakiwa kuwa kiigizo chema na ruwaza njema kwa wasichana wa jinsia yake. Mwanamke atafikia wema vipi? Kila mwanamke anatakiwa atambue kuwa hawezi kufikia wema isipokuwa kwa elimu. Ninayokusudia ni ile elimu ya Kishari´ah anayoisoma ima kutoka katika vitabu – ikiwa yuko na uwezo wa kufanya hivo – au kutoka katika vifua vya wanachuoni. Ni mamoja wanachuoni hawa ni wanaume au wanawake.

Leo imekuwa ni jambo rahisi sana kwa mwanamke kusoma elimu kutoka kwa wanachuoni. Hilo linakuwa kupitia mikanda iliyorekodiwa. Mikanda hii ina nafasi kubwa katika kuielekeza jamii katika yale yaliyo na kheri na wema endapo itatumiwa katika hayo.

Kwa hivyo ili mwanamke awe mwema ni lazima awe na elimu. Hakuna wema isipokuwa kwa elimu. Hivyo asome elimu ima kutoka kwa wanachuoni au kutoka katika vitabu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017