04. Sharti ya nne ya swalah


Sharti ya nne ni mtu kuondosha hadathi, nako ni kule kutia wudhuu´ unaojulikana.

MAELEZO

Kuondosha hadathi inahusiana na ile hadathi kubwa na hadathi ndogo. Ni lazima kwa mswaliji awe msafi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Swalah haikubaliwi pasi na twahara.”[1]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Swalah ya mmoja wenu haikubaliwi anapopatwa na hadathi mpaka atawadhe.”[2]

Hali ya hadathi inaondoshwa kwa maji ikiwa yatapatikana. Ikiwa maji hayakupatikana au yamepatikana lakini hayawezi kutumiwa, basi kunatakiwa kufanywe Tayammum.

[1] Muslim (224).

[2] al-Bukhaariy (135) na Muslim (225).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 64
  • Imechapishwa: 24/06/2018