Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah ina nguzo mbili:

1 – Ukanushaji.

2 – Uthibitishaji.

Makusudio ni kukanusha viumbe vyote vinavyoabudiwa badala ya Allaah (Ta´ala).

Makusudio ya uthibitishaji ni kuthibisha ´ibaadah kwa Allaah (Subhaanah). Yeye ndiye Mungu wa haki. Waungu waliochukuliwa na washirikina wote ni waungu wa batili:

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye wa haki na kwamba vile wanavyoomba badala Yake ndiyo batili.” (22:62)

Imaam Ibn-ul-Qayyim amesema:

“Dalili ya ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` katika kuthibitisha uungu wake ni kubwa kuliko dalili ya maneno yake ´Allaah ndiye Mungu`. Kwa kuwa maneno yake ´Allaah ndiye Mungu` hayakanushi kuabudiwa kwa wengine asiyekuwa Yeye tofauti na kusema ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`. Haya yanapelekea kufanya ustahiki wa kuabudiwa kuwa ni wenye kukomeka na wakati huohuo kuukanusha kwa asiyekuwa Yeye. Hakika amekosea kosa kubwa. Aidha yule aliyefasiri kwamba ´mungu` maana yake ni yule ambaye ni muweza wa kuumba na kuvumbua peke yake.”

Shaykh Sulaymaan bin ´Abdillaah amesema katika maelezo yake ya “Kitaab-ut-Tawhiyd”:

“Mtu akisema: “Maana ya ´mungu` na ´’ibaadah´ imebainika, ni yepi majibu kwa yule mwenye kusema maana ya mungu ni yule ambaye ni muweza wa kuumba na kuvumbua na mfano wa ibara kama hizi, atajibiwa kwa njia mbili:

1 – Maneno haya ni ya kizushi na haitambuliki kama kuna mwanachuoni wala imamu yeyote wa lugha aliyeyasema. Maneno ya wanazuoni na maimamu wa lugha ndio maana ya yale tuliyoyataja kama ilivyotangulia. Kwa hiyo maana hiyo inakuwa batili.

2 – Tukikadiria hivo basi hiyo ni tafsiri yenye inayopelelekea yule Mungu wa haki. Mungu wa haki inapelekea ya kwamba ni lazima awe ndiye Muumbaji Mwenye kuweza kuyavumbua mambo. Asipoweza hayo, basi hawezi kuwa Mungu wa haki hata kama ataitwa mungu. Vilevile malengo si kwamba atayetambua kuwa mungu ni yule ambaye ni muweza wa kuumba atakuwa ameingia katika Uislamu na atakuwa amejipatia funguo za Pepo. Hakuna yeyote anayesema hivi. Hilo litapelekea makafiri wa kiarabu kuwa waislamu. Hata kama tutakadiria kuwa baadhi ya waliokuja nyuma walikusudia hivo, wamekosea. Wanaraddiwa kwa dalili za Qur-aan na Sunnah na za kiakili.”[1]

[1] Taysiyr-ul-´Aziyz al-Hamiyd, uk. 56-57.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´naa laa ilaaha illa Allaah, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 23/09/2023