04. Mwenye kuweka nia ya kufungua swawm inaharibika

3- Swawm inaharibika kwa nia. Yule mwenye kuweka nia ya kufungua swawm yake inaharibika. Haya ndio maoni yenye nguvu zaidi ya wanachuoni. Kwa sababu swawm ni ´ibaadah. Miongoni mwa sharti zake ni kuweka nia kutwa nzima mtu anapokuwa ndani ya ´ibaadah hiyo. Akiweka nia ya kuikata basi ´ibaadah hiyo inaharibika kwa nia na uhakika na hekima ya ´ibaadah hiyo inaondoka. Hivyo swawm inaharibika kwa kukosekana sharti yake kutokana na yale yaliyotangulia:

”Hakika kila kitendo kinategemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia.”

Matendo yamejengwa juu ya nia na ni yenye kuizingatia. Nia ndio yenye kuyafanya yakawa sahihi kwani yanazunguka juu yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 11
  • Imechapishwa: 11/04/2019