36 – Imekuja katika Hadiyth:

”Allaah anapenda kuchemua na anachukia kwenda miayo.”[1]

37 – Allaah anapenda subira.

38 – Allaah anapendezwa na hilo.

39  – Allaah amekwishapanga riziki zote na muda wa kuishi.

40 – Hadiyth inasema kwamba Kifo kitachinjwa.

41 – Allaah anajifakharisha.

42 – Neno, matendo na roho hupanda Kwake.

43 – Hadiyth inasema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisafirishwa mbinguni kwa mwili na roho yake.

44 – Alitazama Peponi a Motoni..

45 – Alifika kwenye ´Arshi bali mpaka juu ya ´Arshi. Kiasi cha kwamba hakukuwa kati yake yeye na Allaah isipokuwa pazia ya Utukufu.

46 – Mitume walidhihirishwa kwake.

47 – Matendo ya ummah wake yalidhihirishwa kwake.

[1] al-Bukhaariy (6223).

  • Mhusika: Imaam Abul-Qaasim Sa´d bin ´Aliy bin Muhammad az-Zinjaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ajwibah fiy Usuul-id-Diyn, uk. 81-86
  • Imechapishwa: 14/06/2021