Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

Ambaye hataki kuwa katika al-Jamaa´ah na akafarikiana nayo, basi ameivua kamba ya Uislamu katika shingo yake na atakuwa ni mpotevu mwenye kupoteza.

Hili ni andiko la Hadiyth:

“Atayefarikiana na al-Jamaa´ah, basi amevua kamba ya Uislamu shingoni mwake.”[1]

Haya ni matishio makali. Ikiwa kwenda kwake kinyume ni katika ´Aqiydah, hii ni kufuru. Ikiwa kwenda kinyume ni katika yasiyokuwa hayo, basi ni upotevu. Kujitenga hakuna kheri yoyote ndani yake. Ima inakuwa ni kufuru au chini ya hapo. Kwa hivyo hakuna kheri katika kujitenga na al-Jamaa´ah. Amesema (Swalla Allaahu ´ayahi wa sallam):

“Jilazimieni na al-Jamaa´ah. Hakika Mkono wa Allaah uko juu ya al-Jamaa´ah.”

Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´ayahi wa sallam) alipomueleza Hudhayfah bin al-Yamaan kuhusu fitina na mfarakano utakaotokea ambapo Hudhayfah akamuuliza: “Unaniamrisha nifanye nini nikikutana na hayo?” Akamwambia:

“Shikamana na al-Jamaa´ah ya Waislamu na kiongozi wao.”[2]

[1] at-Tirmidhiy (2863), Ahmad (04/202/130), al-Haakim (404). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Imaam al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaami´” (1724).

[2] al-Bukhaariy (6673) na (3411) na Muslim (1847).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 15
  • Imechapishwa: 13/06/2017