04. Mavazi sahihi anayotakiwa mwanamke kwenda kuswali nayo ´iyd

Kutokana na yale tuliyonukuu, imepata kubainika kuwa waandishi hawa wanaonelea kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah kwa wasichana kutoka kwenda katika uwanja. Yahifadhi haya. Huenda ikafika siku waandishi hawa kwa sababu ya hasadi na chuki wakapinga yale ambayo siku moja walikuwa wakiyakubali pale watapoona wanusuraji wa Sunnah ni wenye kuitendea kazi Sunnah hiyo.

Sisi hata kama tunawahimiza wanawake kuhudhuria mkusanyiko pamoja na waislamu kwa ajili ya kuhakikisha maamrisho ya bwana wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), haina maana ya kwamba tunapuuzia mavazi ya mwanamke yaliyowekwa katika Shari´ah. Haijuzu kwao kuonyesha kitu katika mwili wao isipokuwa uso na viganja vya mikono, jambo ambalo tumelifafanua katika kitabu “Hijaab-ul-Mar-ah al-Muslimah fiyl-Kitaab was-Sunnah”. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako – na wanawake wa waumini – wajiteremshie Jilbaab zao; hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

Pamoja na kwamba huko tumeweka wazi ya kwamba lililo bora zaidi ni kufunika uso na viganja vya mikono, tofauti na yale wanayoninasibishia baadhi ya waandishi ambao hawamchi Mola wa walimwengu.

[1] 33:59

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swalaat-ul-´Iydayn, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 12/05/2020