04. Mambo manane yanayofunguza


Mambo yanayofunguza ni manane. Nayo ni kama ifuatavyo:

1- Jimaa. Mfungaji ambaye anawajibika kufunga akifanya jimaa mchana wa Ramadhaan basi analazima kulipa siku hiyo na kutoa kafara kubwa; kuacha mtumwa huru, asipopata basi afunge miezi miwili mfululizo, asipoweza basi alishe masikini sitini.

2- Kutoa manii hali ya kuwa macho ima kwa kufanya punyeto, kupapasa, kubusu, kukumbatia au mengineyo mfano wa hayo.

3- Kula au kunywa. Ni mamoja ikawa ni kitu chenye manufaa au chenye madhara kama vile sigara.

4- Kudunga sindano za lishe ambazo zinamtosheleza na chakula. Hizo zina maana ya kula na kunywa. Kuhusu sindano ambazo si za lishe hazifunguzi. Ni mamoja zimetumiwa katika misuli au katika mishipa. Ni mamoja amehisi ladha yake kooni au hakuhisi.

5- Kutia damu kwa mfano mfungaji akatokwa na damu ambapo akatiwa damu kulipizia iliyomtoka. Vilevile kutokwa na damu ya hedhi na nifasi.

6- Kutoa damu kwa kufanya chuku na mfano wake. Ama damu ikitoka yenyewe, kama kutokwa na damu puani, kwa kutoa jino na mfano wake hakufunguzi. Kwa sababu huko sio kufanya chuku wala hakuna maana ya kufanya chuku.

7- Kujitapikisha. Mtu akitapika kwa kutokukusudia hakufunguzi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nubadh fiys-Swiyaam, uk. 04
  • Imechapishwa: 17/05/2018