04. Maana ya kuamini nguzo ya kumuamini Allaah kwa mukhtasari


1- Kumuamini Allaah: Ni kule mtu kuwa na imani ya kukata kabisa ya kwamba Yeye ndiye Mola na mfalme wa kila kitu, kwamba anasifika kwa sifa kamilifu zilizotakasika kutokamana na kila kasoro na upungufu na kwamba Yeye ndiye anastahiki kuabudiwa Mmoja pekee hali ya kuwa hana mshirika. Mtu anatakiwa kuyasimamisha hayo kiujuzi na kimatendo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 07
  • Imechapishwa: 07/02/2018