Allaah (Ta´ala) amesema:

لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“… ili mpate kumcha Allaah.”[1]

Lengo katika Aayah ni kitu ambacho ni lazima kitokee iwapo swawm itatekelezwa kwa njia ya sawa. Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba swawm ina faida nyingi ikiwa ni pamoja vilevile na:

1- Imani inapanda.

2- Uchaji Allaah unapanda.

3- Kumwogopa Allaah kunazidi.

4- Mapambano yanafanyiwa mazoezi.

5- Allaah ameifanya swawm kuwa ni sababu ya mtu kupata afya njema. Kwa ajili hiyo imekuja katika Hadiyth:

“Fungeni mtapata afya njema.”[2]

Usahihi wa Hadiyth umetiliwa maneno.

[1] 02:183

[2] at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw” (8477). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf-ul-Jaami´” (3504).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 10
  • Imechapishwa: 02/06/2017