04. Kumdhukuru Allaah (Ta´ala) mwanzoni wa asubuhi

Allaah (Ta´ala) Anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّـهَ ذِكْرًا كَثِيرًا وَسَبِّحُوهُ بُكْرَةً وَأَصِيلًا

“Enyi mlioamini! Mdhukuruni Allaah kwa dhikri ya wingi. Na Mtakaseni asubuhi na jioni.” (al-Ahzaab 33 : 41-42)

al-Aswiylah” maana yake ni kipindi cha baina ya ´Aswr na Maghrib. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَاذْكُر رَّبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ الْغَافِلِينَ

“Na mdhukuru Mola wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na kwa khofu na si kwa jahara (kunyanyua sauti) katika kauli asubuhi na jioni; na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.” (al-A´raaf 07 : 205)

فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ

“Basi subiri, hakika ahadi ya Allaah ni haki, na omba maghfirah kwa dhambi zako, na msabbih Mola wako kwa Sifa njema jioni na asubuhi.” (Ghaafir 35 : 55)

فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ

“Subiri juu ya yale wanayoyasema, na msabbih kwa Sifa njema Mola wako kabla ya kuchomoza (kwa) jua na kabla ya kuchwa.” (Qaaf 50 : 39)

وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ

“Na wala usiwafukuze wale ambao wanamwomba Mola wao asubuhi na jioni wanataka Uso Wake.” (al-An´aam 27 : 52)

فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ أَن سَبِّحُوا بُكْرَةً وَعَشِيًّا

“Akawaashiria (kwa vile hakuweza kusema) kwamba “Msabihini (Allaah) asubuhi na jioni.” (Maryam 19 : 11)

وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَارَ النُّجُومِ

“Na katika usiku msabbih na zinapokuchwa nyota.” (at-Twuur:49)

فَسُبْحَانَ اللَّـهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ

“Basi Subhaana Allaah (Ametakasika Allaah) wakati mnapoingia jioni na mnapoingia asubuhi.” (ar-Ruum 30 : 17)

وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ

“Na simamisha Swalaah (katika) ncha mbili za mchana na sehemu ya kwanza ya usiku; hakika mema yanaondosha.” (Huud 12 : 114)

16- Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kusema pale kunapoingia asubuhi na kunapoingia jioni:

سبحان الله وبحمده

“Ametakasika Allaah na himdi zote ni Zake.”

mara mia hakuna yeyote atayekuja siku ya Qiyaamah na kitu bora kuliko hicho isipokuwa mtu ambaye amesema mfano wa aloyasema au zaidi.”

17- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inapoingia jioni alikuwa akusema:

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله ، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير ، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر ، رَبِّ أَعـوذُ بِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ وَعَـذابٍ في القَـبْر

“Tumeingia wakati wa jioni na umekuwa Ufalme ni wa Allaah na himdi zote ni Zake Allaah. Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah, hali yakuwa ni Mmoja asiyekuwa na mshirika. Niwake Ufalme na nizake sifa njema na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. Ee Mola! Nakuomba kheri ya usiku huu wa leo na kheri ya baada yake. Ninajikinga Kwako kutokana na shari ya usiku huu wa leo na shari ya baada yake. Ee Mola! Najikinga Kwako kutokana na uvivu na ubaya wa uzee (uzee ubaya). Ee Mola! Najikinga Kwako kutokana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi.”

Alikuwa akisema kunapoingia asubuhi:

أصبحنا وأصبح الملك لله

“Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah… ”

18- ´Abdullaah bin Khubayb amesema:

“Tulitoka katika usiku wenye kunyesha na giza kali ili kumuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atuombee. Tulipomuwahi akasema: “Sema.” Sikusema kitu. Akasema: “Sema.” Sikusema kitu. Akasema: “Sema.” Nikasema: “Ee Mtume wa Allaah! Niseme nini?” Akasema: “Soma mara tatu: “Qul huwallaahu ahad” na Suurat al-Falaq na an-Naas kunapoingia jioni na asubuhi itakulinda kutokana na kila kitu.”

19- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwafunza Maswahabah zake kusema:

“Anapoamka mmoja wenu na aseme:

اللهُمَّ بِكَ أَصْبَحْنَا وَبِكَ أَمْسَيْنَا وَبِكَ نَحْيى وَبِكَ نَمُوتُ وَإِلَيْكَ النُّشُورُ وَإِذَا أَمْسى فَلْيَقُلْ اللهم بك أَمْسَيْنَا وَبِكَ أَصْبَحْنَا وَبِكَ نَحْيى وَبِكَ نَمُوتُ وإِلَيْكَ المصير

“Ee Allaah kwa sababu yako tumeingia katika asubuhi, na kwa ajili yako tumeingia jioni, na kwa ajili yako ndio tumekuwa hai, na kwa ajili yako tutakufa na Kwako tutafuliwa.” Na kunapoingia jioni na anasema: “Ee Allaah kwa ajili yako tumefika jioni, na kwa ajili yako tumefika asubuhi, na kwa ajili yako tuko hai na kwa ajili yako tutakufa na ni Kwako tu marejeo.

20- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Bwana wa Du´aa ya msamaha ni:

اللهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لا إِلهَ إِلاَّ أَنْتَ خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ وَأَنا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ أَبوءُ لَكَ بِنِعْمَتِك عَلَيَّ وأَبوءُ بِذَنْبِي فاغْفِرْ لي فإِنَّه لاَ يغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلاَّ أَنْتَ

“Ee Allaah! Wewe ni Mola wangu. Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe. Umeniumba mimi na mimi ni mja wako. Nami niko juu ya ahadi Yako na agano lako kiasi cha uwezo wangu. Najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya. Nakiri Kwako kwa kunineemesha. Nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unisamehe kwani hasamehi madhambi isipokuwa Wewe.”

Mwenye kuisoma pindi inapoingia jioni na akafa usiku huo huo anaingia Peponi. Mwenye kuisoma pindi inapoingia asubuhi na akafa mchana huo huo anaingia Peponi.

21- Abu Bakr asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sema:

اللهُمَّ عَالِمَ الْغَيْبِ والشَّهَادَةِ فَاطِرَ السَّمواتِ والأَرْضِ رَبَّ كُلِّ شيءٍ وَمَلِيكَهُ أَشْهَدُ أَنَّ لا إِلهَ إِلاَّ أَنْتَ أَعُوذُ بِكَ من شَرِّ نَفْسِي وَشَرِّ الشَّيْطَانِ وَ شِركِه

“Ee Allaah! Wewe ni Mjuzi wa yaliyofichika na yaliyowazi. Wewe ni Muumba wa mbingu na ardhi. Wewe ni Mola wa kila kitu na Mfalme wake. Nashuhudia kwamba hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Wewe. Najilinda Kwako kutokana na shari ya nafsi yangu na shari ya Shaytwaan na shirki yake.”

Katika upokezi mwingine:

وَأَنْ أَقْتَرِفَ عَلى نَفْسي سُوءاً أَو أَجُرَّهُ على مسلم

”Na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea Muislamu.”

Sema hivyo unapoamka asubuhi na unapoenda jioni na pindi unapoenda kulala.”

22- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mja yeyote anayesema mara tatu kila siku asubuhi na jioni:

بِسْمِ اللهِ الَّذِي لاَ يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيء في الأرْضِ وَلاَ في السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ العَلِيمُ
“Kwa jina la Allaah ambaye hakidhuru kwa jina
Lake kitu chochote kile kilicho ardhini wala mbinguni, Naye ni Msikivu na ni Mjuzi.”

isipokuwa hakuna chochote kitachomdhuru.”

23- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa haachi kuomba Du´aa hizi inapoingia asubuhi na jioni:

اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَافِيَةَ فِي الدُّنْيَا والآخِرَةِ اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْعَفْوَ والْعَافِيَةَ في دِيني ودُنْيَايَ وأَهْلِي وَمَالِي اللَّهُمَّ اسْتُرْ عَوْرَاتِي وآمِنْ رَوْعَاتِي اللَّهُمَّ احْفَظنِي بَيْنَ يَدَيَّ وَمِنْ خَلْفِي وَعَنْ يَمِيني وَعَنْ شِمَالِي وَمِنْ فَوْقِي وَأَعُوذُ بِعَظَمَتِكَ أَنْ أُغْتَالَ مِنْ تَحْتِ

“Ee Allaah! Nakuomba msamaha na afya duniani na Aakhirah. Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba msamaha na afya katika Dini yangu, dunia yangu, familia yangu na mali yangu. Ee Allaah! Nisitiri aibu zangu na unitulize khofu yangu. Ee Allaah! Nihifadhi mbele yangu, nyuma yangu, kulia kwangu, kushoto kwangu na juu yangu. Najilinda kwa utukufu Wako kwa kuuawa chini yangu.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 28-34
  • Imechapishwa: 21/03/2017