04. Kukata kucha na kuondosha nywele za kwapani na sehemu ya siri

1. Anayotakiwa kufanya mambo ambayo ni maumbile ya Kiislamu katika mambo ambayo ni maalum kwake na yanafanana na yeye:

a) Kupunguza kucha na kuzipatiliza kwa kuzikata mara kwa mara. Kwa sababu kukata kucha ni Sunnah kwa maafikiano ya wanachuoni. Ni miongoni mwa mambo ya maumbile ya Kiislamu yaliyopokelewa katika Hadiyth. Jengine kuyaondosha ndio usafi na uzuri. Kuyabakiza yakawa marefu kunamfanya mtu akaonekana vibaya na pia kujifananisha na wanyama, kukusanya uchafu chini yake na kuzuia maji kufika chini yake.

Baadhi ya wanawake wa Kiislamu wamepewa mtihani wa kufuga kucha zao kwa ajili ya kujifananisha na wanawake wa kikafiri na kuwa wajinga juu ya Sunnah.

b) Imesuniwa kwa mwanamke kuondosha nywele za kwapani na za sehemu ya siri kwa ajili ya kutendea kazi Hadiyth iliopokelewa katika jambo hilo na kutokana na ule uzuri unaopatikana katika jambo hilo. Lililo bora ni yeye afanye hivo kila wiki au asiziache zaidi ya siku arubaini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 17
  • Imechapishwa: 21/10/2019