4 – Kuhukumu kwa isiyokuwa Shari´ah

Qur-aan imebainisha kuwa kitendo kama hichi ni kufuru na shirki. Pindi shaytwaan alipowazungumzisha makafiri wa Makkah walimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni nani mwenye kusababisha kondoo nyamafu kuwa maiti, akasema: “Allaah.” Ndipo akawafanya wamuulize: “Vile mnavyochinja kwa mikono yenu ni halali na vile anavyochinja Allaah kwa mkono wake mtukufu ni haramu?” Kwa hivyo nyinyi ni bora kuliko Allaah?”[1] Ndipo Allaah akateremsha:

وَلَا تَأْكُلُوا مِمَّا لَمْ يُذْكَرِ اسْمُ اللَّـهِ عَلَيْهِ وَإِنَّهُ لَفِسْقٌ ۗ وَإِنَّ الشَّيَاطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰ أَوْلِيَائِهِمْ لِيُجَادِلُوكُمْ ۖ وَإِنْ أَطَعْتُمُوهُمْ إِنَّكُمْ لَمُشْرِكُونَ

“Wala msile katika wale wasiotajiwa jina la Allaah – kwani huo ni ufasiki. Hakika mashaytwaan wanadokeza marafiki wao wa ndani ili wabishane nanyi. Na mtakapowatii hakika mtakuwa washirikina.”[2]

Katika Aayah hii Allaah (Jalla wa ´Aaa) anaapa ya kwamba yule ambaye atamtii shaytwaan katika Shari´ah yake na kuhalalisha nyamafu ya kwamba ni mshirikina. Inahusiana na shirki kubwa yenye kumtoa mtu katika Uislamu. Haya ni kwa maafikiano ya waislamu wote. Allaah atawatweza wenye kuyafanya hayo kwa kuwaambia:

أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَا بَنِي آدَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ وَأَنِ اعْبُدُونِي ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ

“Je, Sijakukuahidini enyi wana wa Aadam kwamba: “Msimwabudu shaytwaan, hakika yeye kwenu ni adui wa wazi na kwamba [badala yake] mniabudu Mimi pekee – hii ndio njia iliyonyooka.”[3]

Amesema (Ta´ala) kumwambia Ibraahiym:

يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ

“Ee baba yangu! Usimwabudu shaytwaan.”[4]

Bi maana katika kumfuata katika kuweka kufuru na maasi. Amesema:

إِن يَدْعُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا وَإِن يَدْعُونَ إِلَّا شَيْطَانًا مَّرِيدًا

“Hawaombi badala Yake isipokuwa [miungu ya] kike na hawaombi isipokuwa shaytwaan muasi.”[5]

Bi maana hakuna jengine walichokuwa wakikiabudu isipokuwa shaytwaan. Hilo kwa kule kufuata kuchukua Shari´ah zake. Amesema (Ta´ala):

وَكَذَٰلِكَ زَيَّنَ لِكَثِيرٍ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ قَتْلَ أَوْلَادِهِمْ شُرَكَاؤُهُمْ

“Na hivyo ndivyo washirikina wengi walivyopambiwa na washirika wao [wanaowaabudu] kuua watoto wao ili wawateketeze.”[6]

Ameiwaita ´washirika` kwa sababu waliwatii katika maasi ya kuwaua watoto wao.

اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ

“Wamewafanya marabi wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Allaah.”[7]

Pindi ´Adiyy bin Haatim (Radhiya Allaahu ´anh) alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Aayah hiyo, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema kwamba kuwafanya marabi na watawa miungu badala ya Allaah maana yake ni kuwafuata katika kuhalalisha yale aliyoharamisha Allaah na kinyume chake[8]. Hili ni jambo ambalo hakuna tofauti juu yake.

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا

“Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wayakanushe. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa.”[9]

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ

“Na yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.”[10]

أَفَغَيْرَ اللَّـهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ

“Je, nitafute hakimu asiyekuwa Allaah Naye ndiye kakuteremshieni Kitabu kilichopambanuliwa waziwazi? Na wale tuliowapa Kitabu wanajua kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako kwa haki. Hivyo basi, usije kuwa miongoni mwa wanaotia shaka.”[11]

وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚوَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

“Na limetimia neno la Mola wako kwa ukweli na uadilifu – hakuna mwenye kuyabadilisha maneno Yake. Naye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.”[12]

Ukweli ni inapokuja katika maelezo na uadilifu ni inapokuja katika hukumu.

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ

“Je, wao wanataka hukumu za kipindi cha kikafiri? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu; [yanafahamika haya] kwa watu wenye yakini.”[13]

[1] Abu Daawuud (3/245), at-Tirmidhiy (5/246), an-Nasaa’iy (7/237) na Ibn Maajah (2/1059).

[2] 06:121

[3] 36:60-61

[4] 19:44

[5] 04:117

[6] 06:137

[7] 09:31

[8] at-Tirmidhiy (05/259) na amesema:

“Hadiyth hii ni geni.”

[9] 04:60

[10] 05:44

[11] 06:114

[12] 06:115

[13] 05:50

  • Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 13/06/2023