04. Kosa la nne katika ´Aqiydah: Kuapa kwa asiyekuwa Allaah

4- Kuapa kwa asiyekuwa Allaah. Kama mfano wa kuapa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au mtu mwengine na  kuapa kwa amana. Yote hayo ni maovu na ni miongoni mwa mambo ya haramu ya kishirki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwenye kuapa kwa kitu pasi na Allaah basi amefanya shirki.”

Ameipokea Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) kupitia kwa ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Pia ameipokea Abu Daawuud na at-Tirmidhiy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Pia imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

”Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah amefanya kufuru au shirki.”

Pia imethiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

”Msisemi ”Akitaka Allaah na akataka fulani”. Lakini semeni ”Akitaka Allaah kisha akataka fulani”.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Akhtwaau fiyl-´Aqiydah, uk. 3-4
  • Imechapishwa: 21/06/2020