04. Kinga ya nne ya janga la corona: Kuomba du´aa wakati wa kutoka nyumbani

4- Du´aa wakati wa kutoka nyumbani

Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu akitoka kwenye nyumba yake akasema:

بِسْمِ اللهِ تَوَكَّلْتُ عَلى اللهِ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ تَعَالى

“Kwa jina la Allaah. Nimemtegemea Allaah. Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada Allaah (Ta´ala).”

basi hapo huambiwa: “Umeongozwa, umetoshelezwa na kulindwa.” Shaytwaan hujiepusha naye na kuwaambia mashaytwaan wengine:  “Ni vipi mtamuweza mtu ambaye ameongozwa, kutoshelezwa na kulindwa?”[1]

[1] Abu Daawuud.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Ashru Waswaayaa lil-Wiqaayah min-al-Wabaa’, uk. 8
  • Imechapishwa: 30/03/2020