04- Ihram na nia yake


6- Ni wajibu kuhirimia pindi mtu anapofika katika Miyqaat yake. Na wala hilo haliwi kwa ile nia iliyomo moyoni mwake ya hijah, kwa sababu nia haitaacha kuwa moyoni tangu alipotoka nyumbani kwake. Bali ni lazima ima kupatikane kitu au kitendo kitachomfanya awe ni mwenye kuhirimia. Endapo ataleta Talbiyah na akakusudia Ihraam, Ihram yake ni sahihi kwa maafikiano.

7- Mtu asiseme chochote kwa ulimi wake kabla ya Talbiyah. Mfano wa hilo ni pale wanaposema:

“Ee Allaah, nanuia kuhiji au kufanya ´Umrah; nisahilishie kwangu na unikubalie… “

Hakuna chochote katika hayo kilichopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hili ni mfano wa kutamka nia katika twahara, swalah na swawm. Yote hayo ni katika mambo yaliyozuliwa. Inafahamika ya kwamba amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kila kila kitachozuliwa ni Bid´ah, kila Bid´ah ni upotevu na kila upotevu ni Motoni.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 20/08/2017